CRISTIANO Ronaldo nyota wa Juventus inaelezwa kuwa ataendelea kukipiga ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

Habari zilikuwa zinaeleza kuwa Klabu ya PSG ilikuwa sokoni kuisaka saini ya nyota huyo anayekipiga pia timu ya Taifa ya Ureno.


Staa huyo alijiunga na Juventus 2018 akitokea Klabu ya Real Madrid amezidi kuwa bora muda wote ndani ya Juve.

Mkataba wake unameguka msimu wa 2022 hivyo amebakiwa na misimu miwili ndani ya Juventus.


Msimu huu kabla ya Janga la Virusi vya Corona kutibua mambo alikuwa amecheza mechi 32 alitupia mabao 25 na pasi nne za mabao.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.