JUUKO Murshind, beki wa kati anayekipiga ndani ya Klabu ya Wydad Casablanca ya Morroco inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kurejea Bongo mitaa ya Kariakoo huku Yanga ikitajwa kuwa mstari wa mbele kufuatilia nyendo zake.

Beki huyo ambaye alisepa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa anadai stahiki zake huku mabosi wa Msimbai wakisema kuwa alikuwa ametoroka kambini ilikuwa msimu wa 2018/19.

Habari zinaeleza kuwa Yanga inamhitaji Juuko raia wa Uganda arejee Bongo kumpa nguvu Lamine Moro ambaye amekuwa ni mhimili ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael.

"Kwa sasa uongozi upo kwenye hesabu za kuipata saini ya Juuko hivyo mambo yakiwa sawa anaweza kuibukia Jangwani msimu ujao," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mambo mazuri hayahitaji haraka wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.