DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa siku anafanya mazoezi mara tatu ili kulinda kipaji chake pale Ligi Kuu Bara itakaporejea aendelee kuwa kwenye ubora wake.

Nchimbi amesema kuwa amekuwa akiendelea kufanya mazoezi ili kuwa bora kutokana na ligi kusimama kwa sababu ya Virusi vya Corona.

“Wakati huu kwangu ni muhimu kufanya mazoezi ili kulinda kipaji changu ukizigatia kwamba kazi yangu ni mpira, ninafanya mazoezi mara tatu kwa siku ila ninachukua tahadhari pia.

“Program ya mwalimu inatutaka tufanye zoezi mara moja ila wakati mwingine ninajiongeza kwa kufanya zaidi ili kuwa bora kikubwa ni umakini pamoja na tahadhari ,” amesema Nchimbi.

Nchimbi ni mshambuliaji wa kwanza msimu wa 2019/20 kufunga hat trick wakati akikipiga ndani ya Polisi Tanzania na aliwafunga Yanga ambao ni mabosi wake kwa sasa

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.