MOHAMED Rashid, mshambuliaji wa Simba anayekipiga kwa mkopo ndani ya Klabu ya JKT Tanzania amesema kuwa bado hajazungumza na mabosi wake kuhusu hatma ya mkataba wake.
Mo Rashid alisajiliwa na Simba msimu wa 2018/19 akitokea ndani ya Klabu ya Tanzania Prisons ambapo maisha yake ndani ya Simba hayakudumu kwani alitolewa kwa mkopo kukipiga KMC na sasa yupo JKT Tanzania.
Akizungumza na SpotiXtra, Mo Rashid alisema kuwa kwa sasa mkataba wake unakaribia kuisha ndani ya Simba ila hajazungumza na mabosi wake.
“Nipo kwa sasa ndani ya JKT Tanzania na mkataba wangu unakaribia kuisha, msimu ukiisha tu nami namaliza mkataba wangu ila bado sijaitwa mezani kuzungumza na Simba kuhusu mkataba wangu.
“Kwa sasa ninaendelea na mazoezi binafsi nikiwa nyumbani kutokana na kujikinga na Virusi vya Corona nawasihi na wengine waendelee kuchukua tahadhari,” alisema Mo Rashid.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.