JESE Rodriguez, mshambuliaji wa Klabu ya PSG anayekipiga ndani ya Klabu ya Sporting Lisbon kwa mkopo yupo kwenye mpango wa kurejea kwenye klabu yake ya PSG baada ya timu anayoitumikia kwa sasa kotukowa na mpango naye.
Nyota huyo alitimka Real Madrid msimu wa 2016 amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Sporting Lisbon ambapo amecheza jumla ya mechi 17 kwenye mashindano yote.
Wakala wa mchezaji huyo, Gines Carvajal amesema kuwa Jese anahitaji kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo kujifunza ila anashindwa kwa kuwa hayupo kwenye mipango ya timu.
Carvajal anaamini kuwa ili mchezaji awe bora ni lazima acheze mara kwa mara jambo ambalo limekuwa gumu kutokea kwa mteja wake huyo.
" Ni mchezaji mzuri na ana uwezo ndio maana amecheza Real Madrid na PSG na malengo yake ni kucheza klabu yoyote ile inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya," amesema.
Post a Comment