MBARAKA Yusuph, mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona huku akifanya mazoezi binafsi akiwa nyumbani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mbaraka amesema kuwa amekuwa akichukua tahadhari  kulinda afya yake pamoja na wale wanaomzunguka.

"Nipo makini kwa sasa nikichukua tahadhari wakati huu wa maambukizi ya Virusi vya Corona na ninafanya mazoezi ili kuendelea kuwa bora.

"Nina amini wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa na tutarejea kwenye maisha yetu ya kawaida jambo la msingi ni kuchukua tahadhari ili kuwa salama," amesema. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.