SIXTUS Sabilo, mshambuliaji wa Klabu ya Polisi Tanzania amesema kuwa yupo tayari kusaini ndani ya klabu ya Yanga iwapo watafuata utaratibu wa kuipata saini yake.

Sabilo ni miongoni mwa wazawa ambao wanatimiza majukumu yake ipasavyo ambapo ametupia mabao saba msimu huu jambo liloliwavutia mabosi wa Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sabilo ambaye maskani yake ipo Bunda amesema kuwa amekuwa akiskia taarifa za saini yake kuhitajika ndani ya klabu ya Yanga jambo ambalo halijafika mezani.

"Nimeskia kwamba Yanga inanihitaji hilo ni jambo jema kwangu kwani mchezaji lazima awe tayari kuingia kwenye kambi yoyote ile nami sina hiyana iwapo Yanga watahitaji saini yangu kikubwa utaratibu ufuatwe.

"Sio Yanga tu hata Simba, Kagera Sugar ama Lipuli wakifuata utaratibu ninakwenda kucheza bila matatizo, kwa sasa bado nina mkataba na mabosi wangu wa Polisi Tanzania ndipo ambapo nipo kwas sasa,' amesema.

Kwenye mabao hayo saba, Sabilo ameitungia Simba walipokutana Uwanja wa Taifa ambapo mlinda mlango alikuwa ni Beno Kakolanya na ilipokutana na Yanga Uwanja wa Ushirika Moshi aliwatungua Yanga mlinda mlango alikuwa ni Farouk Shikalo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.