UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa tayari ukarabati wa Uwanja wa Azam Complex umekamilika asilimia zote ukiwa sawa na ule wa TP Mazembe.
Akizungumza na SalehJembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa ubora wa uwanja huo kwa sasa ni wa kimataifa.
“Uwanja wetu ubora wake upo sawa na ule Uwanja wa TP Mazembe ya Congo kwa sasa upo hatua ya kimataifa hivyo tunajivunia kukamilisha ukarabati wetu kwa sasa.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona na wakati ukifanyiwa marekebisho Azam FC walikuwa wanatumia Uwanja wa Uhuru na Taifa kwa mechi zao za nyumbani.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.