DARUWESH Saliboko, nyota anayewindwa na Klabu ya Yanga amesema kuwa kwa sasa anapiga mazoezi mara moja kwa wiki ili kulinda kipaji chake.
Nyota huyo anayekipiga ndani ya Lipuli kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa alikuwa kwenye ubora wake ambapo alifunga mabao nane na anatajwa kuwindwa na Yanga.
Saliboko amesema kuwa kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ametenga siku moja kati ya saba kufanya mazoezi.
“Jumamosi ni siku pekee ambayo ninaitumia kufanya mazoezi hii inatokana na kuchukua tahadhari kwani Virusi vya Corona vipo na ni lazima nichukue tahadhari ndio maana ninafanya mara moja pekee,” alisema.
Post a Comment