UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kwa kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya Virusi vya Corona wameamua kuwa mabalozi kwa jamii ili kupambana kwa pamoja kuitokemaza Corona.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wamekuwa bega kwa bega na Serikali katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona kwani ni janga hatari.
“Hili ni janga hatari nasi tumeamua kuungana na Serikali katika kupambana na Virusi vya Corona kwa vitendo ambapo tumekuwa ni mabalozi wa hiyari katika kutoa elimu.
“Kwenye kumbi za burudani tumekuwa tukiwakumbusha kukumbuka kunawa huku tukiwaomba wakumbuke kuwa makini katika kazi zao wanazozifanya kwa kuchukua tahadhari,” amesema Katemana.
Singida United ipo nafasi ya 20 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ambayo kwa sasa imesimamisha kutokana na janga la Virusi vya Corona ikiwa na pointi 15.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.