AISHI Manula mlinda mlango namba moja wa Klabu ya Simba amesema kuwa kwa sasa amezikumbuka kelele za mashabiki wake uwanjani ila anashindwa kuziskia kutokana na kusimamishwa kwa ligi.
Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.
Wakati ligi ikisimamishwa, Simba ikiwa imecheza mechi 28, Manula alikaa langoni kwenye mechi 21 huku zile saba akikaa Kakolanya na aliruhusu jumla ya mabao 10 akiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika ya dakika 189 kwani ametumia dakika 1,890 langoni.
Manula amesema kuwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona kunamfanya ashindwe kuskia kelele za mashabiki kwa kuwa kwa sasa hakuna mechi zinazoendelea.
“Nimekumbuka kurudi uwanjani, nimezikumbuka kelele za mashabiki ila kwa sasa hazipo kutokana na ligi kusimama ni maombi yangu kwa Mungu hili janga la Virusi vya Corona lipite ili tuendelee na shughuli zetu,” amesema.
Post a Comment