OBREY Chirwa mshambuliaji wa Azam FC, ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.
Mkataba wa awali wa nyota huyo alioongeza Juni mwaka jana, ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo kwa kusaini tena kutamfanya aendelee kusalia hadi mwishoni mwa msimu ujao.
Chirwa alikuwa Kwenye hesabu za kurejea Yanga ambayo ilikuwa Klabu yake ya zamani ambayo inaelezwa kuwa walikuwa Kwenye hatua za mwisho kuinasa kwa ajili ya msimu ujao.
Azam FC ikiwa nafasi ya pili na pointi 54 baada ya kucheza mechi 28 imefunga mabao 37 huku Chirwa akitupia mabao nane
Post a Comment