INAELEZWA uongozi wa timu ya APR ya Rwanda umepanga kuvunja mkataba wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ili kuongeza nguvu katika timu yao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Simba inadaiwa kwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutafuta mbadala wake kwa madai ya kuanza kupoteza ubora wake licha ya kuongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 19.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Rwanda zinadai kuwa APR inayomilikiwa na jeshi la nchi hiyo ipo kwenye mkakati mzito wa kuhakikisha inamnasa mshambuliaji huyo. Mtoa taarifa huyo alisema timu hiyo inataka kufika mbali msimu ujao katika michuano ya kimataifa.
“Huo mpango tayari umeshaanza lakini kwanza wamepanga kuanzia kwa kuongeza thamani ya wachezaji wa ndani kisha wapeleke maombi juu ya suala la Kagere maana wamesikia kwamba Simba huenda wakashusha dau lake wanataka kutumia nafasi hiyo ili awasaidie kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao ikiwezekana kupitia viongozi wakubwa wa nchi,” alisema mtoa taarifa.
Meneja wa mchezaji huyo, Patrick Gakumba hakuweza kupatikana kabla ya kupatikana kwa wakala anayefanya kazi ya kuwauzia wachezaji APR, Eto Mupenzi ambaye alisema kuwa : “Nadhani huo mpango wa kuongeza wachezaji thamani na haitokuwa kwa APR kwani itaenda kwa timu zote lakini ishu ya Kagere ni suala la muda na kusubiri”.
Chanzo :Championi
Post a Comment