UONGOZI wa Simba umesema kuwa iwapo nyota wao Clatous Chama anataka kwenda kujiunga na Klabu ya Yanga ni ruksa kwenda.

Kumekuwa na sarakasi nyingi kuhusu usajili wa Chama ambapo Yanga kupitia kwa Makamu Mwenyekiti, Fredrick Mwakalebela alisema kuwa wameanza mazungumzo na Chama kabla ya baadaye kudai kuwa ilikuwa utani.

Pia Simba iliishtaki Yanga kwa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa kudai kuwa Yanga imekiuka utaratibu wa usajili wa FIFA ambao unataka mchezaji kufanya mazungumzo na timu iwapo amebakiza mkataba chini ya miezi sita.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amemruhusu kiungo huyo kujiunga na Yanga.

"Kama Chama anataka kuondoka kwenda Yanga kucheza, milango ipo wazi aende tu akacheze.

"Siyo kwa Chama pekee hata mchezaji mwingine ndani ya Simba akiona hakuna nafasi ya kucheza ruksa kuondoka nafasi ipo wazi," amesema.

Chama alijiunga na Simba msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Power Dynamo ya Zambia mkataba wake inaelezwa unameguka msimu ujao wa 2020/21

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.