UONGOZI wa Yanga umesema kuwa muhimu kwa wachezaji na mashabiki kwa sasa kuendelea kuchukua tahadhari ili kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasihaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kwa sasa hali imekuwa tofauti kutokana na mambo kubadilika hivyo hakuna namna ya kufanya zaidi ya kuchukua tahadhari.
"Muhimu kwa kila mmoja kuchukua ili kuwa salama kwani janga la Virusi vya Corona lipo na kila mmoja anapaswa kuchukua tahadhari ili kuwa salama.
"Tumekumbuka burudani na zile fujo za mashabiki pale tunaposhinda ili turudi huko ni lazima kila mmoja afuate utaratibu uliowekwa," amesema
Post a Comment