HARUNA Niyonzima, raia wa Rwanda anayekipiga ndani ya Yanga kwa sasa amesema kuwa kilichomfelisha kucheza mechi nyingi alipokuwa ndani ya Simba ni majeraha.

Alipokuwa akikipiga Simba msimu wa 2018/19 akiwa chini Kocha Mkuu, Patrick Aussem alikaa nje ya Uwanja nusu msimu.

"Nilikuwa kwenye ubora wangu pia ndani ya Simba lakini nilishindwa kufanya vizuri kutokana na tatizo la majeraha jambo lililonifanya nisionyeshe makeke mengi.


"Kifundo cha mguu kiliniweka nje kwa muda wa nusu msimu na hiyo ni sababu ya kufanya nisifanye vizuri ila nina amini katika uwezo wangu," amesema Niyonzima.

Kwa sasa Niyonzima anakipiga ndani ya Yanga ambayo alijiunga nayo kwenye dirisha dogo akitokea AS Kigali timu yake ipo nafasi ya tatu na imejiwekea kibindoni pointi 51 kwenye mabao 31 waliyofunga yeye amefunga bao moja.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.