ETIENNE Ndayiragije, Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” amefanya mabadiliko katika kikosi kutokana na baadhi ya wachezaji kuwa majeruhi.

Wachezaji walioondolewa katika kikosi kwa sababu ya kuwa majeruhi ni David Mwantika,Aishi Manula na Ibrahim Ajibu ambao nafasi zao zimezibwa na Mohamed Ally Yusuf(Lipuli),Oscar Godfrey Masai(Azam FC) na Haruna Shamte(Lipuli).

Stars itamenyana na Kenya Agosti 4 kwenye mchezo wa marudio wa kufuzu michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika Cameroon 2020.
Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.