LUIS Miquissone ameibua mapya ndani ya Simba baada ya uongozi kusema kuwa ulichelewa kumtambua nyota huyo.
Luis aliyejiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea UD Songo, Februari 22 alifunga bao lake la kwanza ndani ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa dhidi ya Biashara United.
Simba ilishinda mabao 3-1 huku bao la pili lililofungwa na Meddie Kagere yeye akitoa pasi ya mwisho na bao la tatu lilifungwa na Kahata Francis kwa pasi ya Jonas Mkude.
Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema:-"Wanasimba kwa wanafurahi kwa kuwa soka safi linachekeza na burudani inatolewa, watazamaji wanalipa viingilio halali kabisa.
"Miquissone kwa nini tulichelewa kukujua wewe ni sawa na Messi (Lionel).
Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 62 imecheza mechi 24
Post a Comment