ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wamejipanga kuona wanapata ushindi mbele ya Ndanda FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Gairo.
Mwezi Februari, Mtibwa Sugar haijashinda mchezo kwenye mechi saba mfululizo ikiambulia pointi moja kati ya 21 ikiwa leo itafungwa itaacha jumla ya pointi 23 kwenye ligi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa watapambana kwenye mechi zinazofuata, matokeo yote yaliyopita haiwekezakani kuyabadilisha kwa kuwa yametokea.
“Ukishafungwa ama kupata sare hakuna unachoweza kukibadilisha zaidi ni kutazama namna gani timu ilifanya makosa na kuyarekebisha ili kuwa bora na kupata matokeo mazuri, mechi zetu nyingine tutapambana kupata matokeo,” amesema Katwila.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 24 imecheza mechi 24 itamenyana na Ndanda iliyo nafasi ya 14 na pointi zake 26.
Post a Comment