GEOFREY Luseke, beki wa timu ya Alliance amesema kuwa hawakustahili kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wapinzani wao Yanga.
Jana, Februari 29, Alliance ya Mwanza ilikubali kichapo kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Luseke amesema:'Haikuwa mipango yetu kupoteza mbele ya wapinzani wetu Yanga ila kutokana na wao kutumia makosa yetu basi wameweza kutushinda kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zinazokuja," .
Alliance FC ipo nafasi ya 13 imejikusanyia pointi 29 kibindoni baada ya kucheza mechi 25.
Post a Comment