DEAN Smith, Kocha Mkuu wa Aston Villa amesema kuwa ana imani na mchezaji wake Mbwana Samatta atakuwa na msaada ndani ya timu hiyo kwenye mchezo wa Jumapili, Machi Mosi, utakaochezwa Uwanja wa Wembeley.
Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania amecheza mechi nne ndani ya timu yake mpya ya Aston Villa aliyojiunga nayo akitokea Klabu ya Genk na anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo huo wa fainali ya Kombe la Carabao itakapomenyana na Manchesterc City.
Villa ilipenya kwenye hatua ya fainali baada ya kuishushia kichapo Leicester City kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya ule wa kwanza kufungana bao 1-1.
"Anazidi kuimarika kadri anavyocheza na uwezo wake unazidi kuwa bora kwani kadri unavyocheza unakuwa imara, akiongeza juhudi atakuwa bora zaidi," amesema.
City na Villa zimekutana mara 171 kwenye michuano yote ambapo Villa imeshinda mechi 57, City imeshinda mechi 73 na sare 41 hivyo mchezo huo wa 172 utakuwa ni wa kukata na shoka.

Post a Comment