LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa licha ya kuachwa mbali na wapinzani wao Simba haitawafanya wawe wanyonge pindi watakapokutana uwanjani.
Machi 8, Uwanja wa Taifa Yanga itaikaribisha Simba kwenye mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara baada ya ule wa kwanza ambapo Simba ilikuwa mwenyeji kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa wameachwa mbali na wapinzani wao Simba ila haiwafanyi wawe na hofu kucheza nao kwenye mchezo wao watakapokutana.
“Ligi ni ngumu na kwetu kila mechi inakuwa na changamoto zake hivyo ninachokifanya ni kuwapa majukumu wachezaji wao wayatimize ndani ya uwanja kwani siwezi kuingia, kuhusu kuachwa na wanaoongoza ligi kila mtu anajua lakini haitatufanya tuingie uwanjani tukiwa wanyonge, hapana haiwezi kutokea.
“Kinachotoa matokeo ni juhudi za wachezaji kufuata kile ambacho ninawaelekeza na kushirikiana, ninawaona vijana wangu wana nguvu ila tatizo lao ni kwenye umaliziaji hilo likiisha basi mashabiki watapenda na watafurahi,” amesema Eymael.
Yanga ipo nafasi ya nne kwenye Ligi ikiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 22 ina mechi mbili mkononi kuifikia Simba yenye pointi 62 na imecheza mechi 24 ikiachwa kwa pointi 21.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.