LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa maandalizi ya mchezo wa leo dhidi ya Gwambiana FC yapo vizuri wanaamini watapata ushindi utakaowapa nafasi ya kusonga mbele.

Yanga leo itamenyana na Gwambina kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora utakaochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.

Mchezo huu ni wa Kombe la Shirikisho na bingwa mtetezi ni Azam FC iwapo itashinda leo itatinga hatua ya robo fainali.

Eymael amesema :' "Tupo vizuri na maaandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa, ninaamini kwamba wachezaji watatimiza majukumu yao ipasavyo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu,".

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.