MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Azam FC wamesema kuwa mpango wao mkubwa ni kuona wanaweza kulitetea taji hilo ili wakwee pipa kuiwakilisha nchi kimataifa.

Azam FC jana Februari 25 ilipenya hatua ya robo fainali baada ya ushindi wa penalti 5-4 mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Ihefu ulikuwa mgumu ila walipambana na kupata matokeo jambo linalowapa nguvu ya kuendelea kutimiza malengo.

"Haikuwa kazi rahisi kwa kuwa tumetinga hatua ya robo fainali basi malengo yetu ni kuona tunalitwaa taji na kurejea tena kimataifa, nafasi ipo na wachezaji wapo vizuri tunawaomba mashabiki watupe sapoti,"amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.