SHIZA Kichuya amesema kuwa mechi yao dhidi ya Stand United ilikuwa ngumu kutokana na hatua ambayo walikuwa wanacheza na asili ya mashindano kuwa ni zaidi ya fainali na ni michuano migumu.

Kichuya amesema kuwa haikuwa kazi nyepesi kwa timu ya Simba kupenya hatua ya robo fainali kutokana na upinzani ambao walikutana nao kwa wapinzani wao.

Mchezo huo wa hatua 16 bora Kombe la Shirikisho ulichezwa Uwanja wa Kambarage na Simba ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa kufungana bao 1-1.

"Kombe la Shirikisho ni tofauti na makombe mengine hapo ukifungwa unatolewa jumlajumla sasa kila timu inaingia ikiwa na mbinu kali za kutafuta ushindi maana ile ni fainali na ili iwe fainali lazima ushindani uwepo," amesema.

Simba imerejea jana Februari 26 Bongo baada ya kucheza na Stand United Shinyanga Februari 25 mchezo wake unaofuata ni Machi Mosi dhidi ya KMC.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.