CLATOUS Chama, kiungo ndani ya Simba amesema kuwa watapambana kufikia malengo waliyojiwekea ndani ya Simba kwa pamoja.
Chama jana alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi kilichoshinda mbele ya Stand United kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho mbele ya Stand United Uwanja wa Kambarange.
Ndani ya dakika 90 Simba ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na ilipenya kwa penalti 3-2 imetinga hatua ya robo fainali.
"Tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye mashindano ambayo tunashiriki na hapa ambapo tupo kwenye Kombe la Shirikisho, imani yetu ni kuona tunafanya vizuri na kupata matokeo, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Post a Comment