UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa nyota wao Salum Kihimbwa amerejea rasmi uwanjani kutokana na kupona majeraha yake.

Kihimbwa alikuwa nje ya kikosi hicho cha Mtibwa kilicho chini ya Zuber Katwila tangu Februari 2.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wana imani anaweza kucheza mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC.

Kwenye mechi saba ambazo Mtibwa Sugar wamecheza mwezi Februari imekuwa ngumu kufurukuta kwa kupata matokeo kwani wamepoteza mechi sita na kuambulia pointi moja.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.