JOHN Bocco nahodha wa Simba amefunga mabao matatu ambayo yameacha gumzo ndani ya Bongo kutokana na kufunga mabao yake kwa miguu yote miwili ya kulia na kushoto huku akifunga kwa kutumia mguu wa mwisho ambao  amepewa pasi.

Yaani kwenye mabao yake matatu mchezaji wa mwisho akimpa pasi kwa mguu wa kulia naye anafunga kwa mguu wa kulia na akipewa kwa mguu wa kushoto anafunga pasi kwa mguu wa kushoto.

Bao la kwanza alifunga Uwanja wa Taifa kwa mguu wa kulia kwa pasi ya Clatous Chama aliyotengewa kwa guu la kulia dakika ya 57, ilikuwa Februari 4.

Bao lake la pili alifunga mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri , Februari 11 alifunga dakika ya 45 kwa guu la kushoto kwa pasi ya Meddie Kagere aliyotengewa kwa guu la kushoto na kupachika bao lake la pili msimu huu, 

Simba ilishinda kwa mabao 3-0. Pia alitoa pasi ya kwanza kwa guu la kulia iliyoleta bao lilifungwa na Hassan Dilunga kwa guu la kulia.

Februari 15 alipachika bao lake la tatu na la ushindi kwa Simba mbele ya Lipuli na Simba ilishinda kwa bao 1-0 na kusepa na pointi tatu Uwanja wa Samora, Iringa, alifunga kwa guu la kushoto dakika ya 22 alipewa pasi kwa guu la kushoto na Francis Kahata mwenye jumla ya pasi nne za mabao na amefunga pia mabao sita..

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.