UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kesho utapambana kupata matokeo mbele ya Gwambina kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Yanga itawakaribisha Gwambina saa 1:00 usiku kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wana imani ya kurejea kwenye ubora wao kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya.
"Kikosi kilirejea mapema kutoka Tanga kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Gwambina, ni timu bora hilo tunatambua ila itakutana na timu kubwa na yenye wachezaji wenye uzoefu.
"Mpira una ushindani na kila timu inahitaji ushindi ndivyo ilivyo na kwetu pia tunahitaji ushindi," amesema.
Yanga ilitinga hatua ya 16 bora baada ya kuichapa mabao 2-0 Tanzania Prisons hatua ya 32 bora Uwanja wa Taifa.
Post a Comment