Jay
Deas ambaye Kocha Mkuu wa bondia Deotnay Wilder amesema alimkataza
msaidizi wake Mark Breland ambaye ni bingwa wa zamani wa dunia kutupa
taulo ulingoni wakati Wilder akichakazwa na Tyson Fury katika raundi ya
saba ya pambano la uzito wa juu.
Wilder
ametangaza kumfuta kazi Breland akisisitiza alivunja makubaliano kwa
kuwa walishakubaliana tokea mwanzo, hata apigwe vipi, yeye ni shujaa na
mpambanaji na asingependa suala la kurushwa taulo hadi mwisho.
Deas
amesema alimkataza Brealand kufanya hivyo hata kama Wilder alikuwa
akipigwa vipi lakini hakusikia na kuamua kurusha taulo hiyo iliyomaliza
pambano katika ukumbiwa MGM Grand Arena nchini Marekani.
Kwa
sasa mabondia hao wako katika harakati za kuangalia kama wanaweza kuwa
na pambano la marudiano likiwa la tatu kwa kuwa la kwanza walitoka sare
na la pili, Fury kutoka Uingereza akashinda kwa TKO katika raundi ya
saba.
WILDER AKIJIFUA NA BRELAND |
Post a Comment