SHIZA Kichuya, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anaamini ataingia kwenye mfumo wa kikosi muda si mrefu kutokana na kushindwa kuonyesha makeke kwenye mechi nne za hivi karibuni.

Akiwa ndani ya kikosi cha Simba amecheza dakika 45 kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania na timu yake ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 hakucheza mbele ya Mtibwa Sugar, Lipuli, Kagera Sugar na Biashaa United.

"Nipo ndani ya timu kwa sasa ni mfumo tu bado haujanikubali wakati tayari umeshaanza kuzungumza ni sauala la muda tu kurejea uwanjani na mwalimu ninajua ana mbinu zake na aina ya wachezaji anaowataka nimeanza kurejea kwenye ubora," amesema.

 Kichuya amejiunga na Simba kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Klabu ya Pharco FC ya Misri.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.