KIKOSI cha Simba leo kimetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa penalti 3-2 mbele ya Stand United kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Uwanja wa Kambarage.

Dakika tisini zilikamilika kwa Stand United kusawazisha bao dakika ya 67 kupitia kwa Miraj Saleh aliyesawazisha bao la Simba lililofungwa na Hassan Dilunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51.

Penalti kwa upande wa Simba zilifungwa na Clatous Chama, Deo Kanda na Hassan Dilunga huku Meddie Kagere na Ibrarahim Ajibu wakikosa penalti zao.

Kwa upande wa Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza licha ya kumaliza mpira ikiwa pungufu kufuatia mchezaji wao Mwente kuonyeshwa kadi nyekundu ilikaza.

Ilifunga mabao mawili kupitia kwa Brown Raphael na Juma Ndaki

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.