KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wapinzani wao Gwambina walikaza mwanzo mwisho na waliufanya mchezo kuwa wa kukimbizana jambo lililokuwa likiwapa ugumu wa kushindwa kufunga mabao mengi ila mpango wao wa kupata matokeo ulifanikiwa.

Yanga jana iliifungashia virago Gwambina FC kwa ushindi wa bao 1-0 lililopachikwa na Haruna Niyonzima aliyetupia bao hilo dakika ya 45 akiwa nje ya 18, Uwanja wa Uhuru.

"Tunashukuru kwa kuwa tumepata ushindi, wapinzani wetu walikuwa na spidi na walifanya mchezo uwe wa kukimbizana mwanzo mwisho uwanjani, ila hilo hatujali tumepata matokeo na hilo lilikuwa lengo letu," amesema.

Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho inasubiri kuchezwa droo ili kutambua wapinzani wao watakaokutana nao kwenye hatua hiyo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.