SVEN Vandenbroeck Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna tatizo kubwa kwenye safu yake ya ulinzi jambo ambalo atalifanyia kazi kwa ukaribu.
Simba jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na kushinda kwa penalti 3-2 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho licha ya kuanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 51 kupitia kwa Hassan Dilunga.
Sven amesema:" Wachezaji wanajituma ila nimegundua kuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji ni makosa ambayo tuliyafanya na tukaenda kuibukia kwenye penalti wakati mwingine tunak kazi ya kurekebisha makosa yetu,".
Bao la kusawazisha kwa upande wa Stand United lilifungwa dakika ya 67 na Miraj Saleh baada ya beki wa Simba kujichanganya.
Post a Comment