HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kutinga kwao hatua ya robo fainali mbele ya Gwambina kunawapa muda wapinzani wao kurejea Mwanza kuendelea na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kucheza ngoma.

Februari 26 Yanga ilitinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Gwambian FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Haruna Niyonzima dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa nye ya 18.

Bumbuli amesema:-"Hatukuwa na matokeo mazuri ila tulipambana na kupata ushindi mbele ya Gwambina, kwa ushindi huo inatoa fursa ya kusonga mbele huku wapinzani wetu Gwambina wao wakirudi kwenye Ligi Daraja la Kwanza na kuendelea na utamaduni wao wa kucheza ngoma kama ambavyo tuliwaona,".

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.