KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abadlah Mohamed 'Bares' amesema kuwa walishindwa kupenya hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kutokana na kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata.
Alliance ilishinda jana kwa mikwaju 5-3 ya penalti dhidi ya JKT Tanzania na kuifungashia virago timu hiyo.
Licha ya JKT Tanzana kuanza kufunga bao la kuongoza lilisawazisha na Alliance na kufanya dakika tisini zikamilke kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Bares amesema:"Tumepambana kwa kadri ya uwezo wetu mwisho wa siku tumeshindwa kupata matokeo na timu imepoteza ila kwa kuwa penalti hazina mwenyewe basi tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu za Ligi Kuu Bara," amesema.
Post a Comment