LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikosi kwa sasa bado kipo kwenye presha kubwa kutokana na matokeo ambayo wanayapata.

Eyamel amekiongoza kikosi chake kupata sare nne mfululizo ndani ya Ligi Kuu Bara na kufunga mabao mawili ilikuwa mbele ya Mbeya City 1-1, Prisons 0-0, Polisi Tanzania 1-1 na Coastal Union 0-0.

Yanga ipo nafasi ya nne ikiwa imekusanya pointi 41 baada ya kucheza mechi 22 huku vinara wakiwa ni Simba wenye pointi 62 na wamecheza mechi 24.

Eymael amesema:"-Matokeo ambayo tunayapata yanatuweka kwenye presha kubwa kwa sababu hayafurahishi na wala hayapo kwenye malengo yetu kwa kweli.

“Ninajua mashabiki wanaumia na matokeo yetu jambo ambalo siyo zuri kwa sababu presha inakuwa kubwa kila baada ya mechi na tuna kazi ngumu ya kufanya," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.