PIERRE -Emerick Aubameyang amesema kuwa amekosa furaha kwa timu yake kushindwa kupenya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa kwa kufungwa mabao 2-1 na Olympiacos.

Pape Abou Cisse alifunga bao la kuongoza dakika 53 na kufanya matokeo kuwa 1-1 kutokana na ushindi walioupata Arsenal mchezo wa kwanza kwa kufungwa bao moja ugenini.

Kwenye dakika za nyongeza, Aubameyang alifunga bao dakika ya 113 na bao la ushindi lilifungwa na Youssef El-Arabi dakika ya 119 na kufanya ubao uwe 2-1 na kupenya kwa ushindi wa bao la ugenini.

Aubameyang amesema: " Sijui inakuaje, sina furaha katika hili, kufungwa na kutolewa hatua hii kwangu ni mbaya na kwenye timu pia sijapenda na sijafurahi hali hii.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.