LEO Februari 29 Yanga itawakaribisha Alliance kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Rekodi zinaonyesha kwamba Alliance iliyopanda Daraja msimu wa 2018/19 haijaambulia pointi mbele ya Yanga na ilianza kukutana na balaa Heritier Makambo na ocha Mkuu, Mwinyi Zahera.
Aliance iliyo chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro itakutana na Yanga inaliyoandamwa na matokeo ya sare kwenye mechi zake nne za ligi ilizocheza.
Kwenye mechi tatu ambazo wamekutana, Yanga imefunga mabao sita na imefungwa mabao mawili na Alliance, kwenye mchezo wao wa msimu huu Novemba 29 Yanga ilishinda mabao 2-1 hivyo leo Alliance watakuwa na kazi ya kulipa kisasi.
Matokeo yao yalikuwa namna hii:-Oktoba 2018 Uwanja wa Taifa, Yanga 3-0 Alliance, Machi 2, 2019 Alliance 0-1 Yanga Uwanja wa CCM Kirumba.
Post a Comment