UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kosa lao kubwa ilikuwa kuzifunga Simba na Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi jambo lililowafanya wakamiwe na timu nyingine wanapocheza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa timu nyingi zimeanza kuwapigia hesabu kali kwa kucheza nao kwa kukamia jambo linalowapa matokeo mabovu.

"Tuliposhinda Kombe la Mapnduzi kwa kuwafunga vigogo Simba na Yanga hapo ndipo matatizo yalipoanzia, timu nyingi zilianza kucheza nasi kwa kutukamia jambo lililofanya mechi zetu zote kuwa ngumu.

"Wachezaji nao walikuwa na kazi ya kufanya ila walishindwa kupata matokeo mazuri, ni mbaya kwetu na inaumiza ila tutapambana kurejea kwenye ubora wetu," amesema. 

Mtibwa Sugar ilitwaa taji la Mapinduzi kwa kuifunga Simba bao 1-0 kwenye fainali na ilitinga hatua ya fainali kwa kuinyoosha Yanga kwa mikwaju 3-2 ya penalti baada ya sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.