SHIZA Kichuya, kiungo ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa mchezaji mwenzake, Luis Miquissone ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kufanya maamuzi jambo ambalo litaipa manufaa timu ya Simba.
Luis amesajiliwa na Simba kwenye dirisha dogo la usajili akitokea UD Sngo ya Msumbiji mguuni ana bao moja na pasi moja ya bao yote aliyafanya kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 3-1.
Kichuya amesema:-"Luis ni mchezaji mzuri, ambaye amekuwa na utimamu mzuri wa mwili lakini pia ana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira mguuni, akiendelea katika kiwango hiki na akiwa anapata nafasi ya kucheza atakuwa msaada ndani ya timu.
“Imekuwa bahati kwake pia amekuja kipindi kizuri, timu inacheza vizuri na amekuwa akipata bahati ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza, hivyo namuona akifika mbali kama atakuwa na nidhamu hii kwa kipindi chote,” amesema.
Post a Comment