KOCHA Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa mpango wake mkubwa msimu huu ni kuwauza nyota wake nane ndani ya kikosi hicho.
Lampard ambaye aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Chelsea na alifundishwa na Jose Mourinho ambaye ni Kocha Mkuu wa Spurs inayoshiriki Ligi Kuu England ila walipokutana naye msimu huu kwenye mechi zao za ligi alimpiga nje ndani mwalimu wake.
Miongoni mwa wachezaji ambao amepanga kuwauza ni pamoja na Kepa Arrizabalaga,Ross Barkley na Jorginho hawa wapo kwenye hesabu za kuuzwa msimu huu.
Marcos Alonso, Emerson, Kurt Zouma, Willian na Pedro ni miongoni mwa nyota hao anaotarajia kuwauza kutokana na kile anachoeleza kuwa wameshindwa kutimiza majukumu yao kwa ukamilifu.
Post a Comment