NAMUNGO FC jana imetinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa ushindi huo umetokana na wachezaji wake kujituma na kufanya kazi kwa bidii ndani ya uwanja jambo linalomfanya afurahi.

"Ni kazi nzuri vijana wangu wamefanya bado nina imani wataendelea kufanya hivi kwenye mechi zetu zinazofuata.

"Wanatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu ikipata matokeo nao wanapambana kushinda kwa hilo ninawapongeza, " amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.