Bondia Deontay Wilder amesema vazi alilovaa wakati akiingia ulingoni kuzichapa na Tyson Fury raia wa Uingereza, lililichangia yeye kupigwa.

Wilder raia wa Marekani ambaye hakuwa amewahi kupigwa alipoteza pambano lake la kwanza katika raundi ya saba kwa kuchapwa kwa KO baada ya kocha wake kurusha taulo ulingoni.



Wilder amesema kwa muda mwingi alijisikia miguu yake haina nguvu na anaamini uzito wa vazi lile lililokuwa likimuonyesha kama jitu la kutisha lilichangia sana.


"Kuanzia raundi ya pili nilisikia sina nguvu, hakika niliumia sana. Niliona kila kitu hakiwezekani lakini ndio hivyo imepita na ninataka kuanza upya tena," alisema Wilder.


Tayari Wilder na timu yake wameomba pambano la tatu ambalo litakuwa ni la kumaliza ubishi dhidi ya Fury.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.