UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wapinzani wao Ihefu walionyesha ushindani jambo lililowapeleka mpaka hatua ya kupigiana mikwaju ya penalti.
Kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya ndani ya dakika 90 timu zote zilitoshana nguvu kwa kutofungana na mshindi Azam FC alipatikana kwa mikwaju ya penalti na alishinda penalti 5-4.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wachezaji walipambana mwanzo mwisho na walikutana na ushindani mkubwa jambo lililowapeleka kufika hatua ya penalti.
"16 bora ya kuitafuta robo fainali ilikuwa ngumu na yenye ushindani, linapokuja suala la kucheza na bingwa mtetezi timu nyingi huwa zinatambua kwamba zinacheza na timu bora hivyo mipango yao huwa inakuwa imara sababu hizo zilitufanya tufike hatua ya penalti ila tumeshinda na wapinzani wetu walikuwa imara," amesema.
Post a Comment