UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hesabu zao za kuendelea kuutafuta ubingwa kwa sasa zipo mikononi mwa JKT Tanzania itakapomenyana nao leo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Azam FC ipo nafasi ya pili ina pointi 45 kibindoni ikiwa tofauti ya pointi 17 na Simba iliyo nafasi ya kwanza yenye pointi 62 zote zimecheza mechi 24.
Akizungumza na Saleh Jembe, Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kasi yao ilipunguzwa nyanda za juu Kusini kwa kufungwa na kutoa sare kwenye mechi zao mbili.
“Nyanda za juu Kusini hatukufanya vizuri kwani mechi zetu mbili tulishindwa kushinda, tulipata sare na Ndanda FC kisha tukapoteza mbele ya Namungo, lakini haina maana kwamba ligi imekwisha bado tupo na tunapambana mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania utaturudisha kwenye reli,” amesema.
Post a Comment