Home
Unlabelled
KUMEKUCHA, SIMBA KUPOKEA UGENI LEO KUTOKA UJERUMANI UTAKAOWACHEKI WAKIMENYANA NA YANGA
JOTO la mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba limeanza kupanda ambapo kwa sasa timu ya Simba leo inatarajia kuwa na ugeni kutoka nchini Ujerumani ambao utapata fursa ya kuucheki mtanange huo.
Ugeni huo ni maalumu kwa ajili ya timu ya Wanawake Simba Queens ambayo inashirki Ligi ya Wanawake unatarajiwa kuingia leo kutoka nchini Ujerumani ni timu ya Wanawake ya St.Paul.
Itakuwa nchini kwa muda wa siku 15 na inafanya ziara maaluu yenye lengo la kuhamasisha usawa wa kijinsia.
Timu hiyo Ikiwa nchini itashiriki shughuli mbalimbali za kijamii, kufanya utalii visiwani Zanzibar na kwenye hifadhi ya Mikumi lakini pia watapata nafasi ya kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu ambao utapigwa Machi 8, 2020 dhidi ya Yanga.
Post a Comment