DAVID De Gea mlinda mlango wa Manchester United huenda akauzwa ili kuiongezea timu yake mkwanja wa kufanyia usajili msimu huu.
De Gea mwenye miaka 29 raia wa Hispania amekua akifanya makosa ya mara kwa mara ambayo yanaigharimu timu yake kushindwa kupata matokeo mazuri.
Juventus na PSG zinapewa nafasi ya kuinasa saini ya nyota huyo wa Manchester United.
Mkataba wake ndani ya United unatarajiwa kumeguka mwaka 2023.
Post a Comment