UONGOZI wa Klabu ya Yanga, leo Februari 25, 2020 umezungumza na wanahabari baada ya timu hiyo kutoka sare katika michezo yake minne ambayo imewafadhaisha mashabiki wake.
Aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Jerry Cornell Muro, leo ameibuka makao makuu ya timu hiyo Mtgaa wa Jangwani, Kariakoo, na kuongea na wanahabari kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Gwambina FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako amesema:
“Wana Yanga kesho twendeni uwanjani kwa uwingi. Ujio wangu leo ni ujio maalumu ambao umenileta hapa kuja kuleta ‘password’. Habari ya Yanga kupoteza michezo yake msahau, kila kitu kimewekwa sawa. Benchi la ufundi, kocha wachezaji mambo ni fresh. Tumeongea na kocha tumekubaliana kuanzia kesho hatutaki ushindi wa magoli machache, tunataka ushindi wa magoli matatu, manne, nane na kuendelea.
“Matokeo hayo yanapatikanaje? Anajua yeye maana ametoka Ulaya amekuja Tanzania kufundisha mpira, tunataka ushindi. Nimeleta password tunajua tumehujumiwa sana kwenye mechi zetu, wao walikuwa wanapita hapohapo na kuvuruga mipango yetu nasema hujuma sasa basi
Post a Comment