UONGOZI wa Simba umesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wao dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Machi Mosi.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wanatambua kuwa wanakutana na timu bora ila wao pia wamejipanga kupata ushindi kwenye mchezo huo.

"Mchezo wetu unaofuata na tunaoutazama kwa sasa ni dhidi ya KMC, ninatambua kuwa ni timu nzuri na ina ushindani mkubwa ila hilo sio juu yangu ninachotazama mimi ni kwa upande wa timu yangu kupata matokeo.

"Mchezo utakuwa mgumu nimewaambia wachezaji kuwa kazi yetu ni kutafuta matokeo uwanjani na sio kuleta sababu," amesema.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa , KMC ilikubali kufungwa mabao 2-0 na kuziacha pointi tatu zote kwa Mnyama.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.